KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 19, 2010

Armand Traore KUONDOKA ARSENAL.


Arsenal wapo katika taratibu za mwisho za kumuuza beki wao wa kushoto toka nchini Ufaransa Armand Traore kwenye klabu ya Benfica, ya huko nchini Ureno.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 20 anatarajia kuondoka Arsenal kwa ada uhamisho wa Euro million 4 ambazo ni sawa na paund million 3.2.

Itakumbukwa kuwa Arsene Wenger alimsajili Traore akiwa na miaka 16 akitokea AS Monaco ya nchini Ufaransa mwaka 2005, na mwaka 2008 alimuuzwa kwa mkopo katika klabu ya Portsmouth na kisha alirejea Emirates mwaka 2009.

Sababu kubwa ya kutarajia kuondoka Emirates kwa mchezaji huyo ni kufuatia kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza ambacho mara kadhaa kimekua kikitumikia na Gael Clichy pamoja na Kieran Gibbs.

No comments:

Post a Comment