KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

ARTETA ANENA BAADA YA .....


Kiungo wa kimataifa toka nchini Hispania Mikel Arteta Amatriain ameonekana kufurahishwa na hatua ya uongozi wa klabu yake kumzawadia mkataba mpya ambao utamuwezesha kuendelea kuwepo klabuni hapo kwa miaka mingine mitano.

Mikel Arteta amesema hatua hiyo ni faraja kwake na amejihisi bado anathaminika huko Goodson Park alipodumu kwa muda wa miaka mitano iliyopita toka aliposajiliwa mwaka 2005 akitokea Real Sociedad.

Amesema kufuatia hatua hiyo ameendelea kujisikia ni mwenye furaha klabuni hapo na mwisho wa siku anatambua kazi yake ni kuwalipa fadhila viongozi wa Everton kwa kucheza soka la kujituma zaidi na kuifanya klabu iwe miongoni mwa vilabu vinavyofikia malengo yaliyowekwa.

Itakumbukwa kuwa kabla ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 hajasainishwa mkataba mpya, alikuwa nawania na klabu za Tottenham Hotspur, Aston Villa pamoja na Manchester City.

No comments:

Post a Comment