KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 13, 2010

ARSENAL KUSHUKA DIMBANI PUNGUFU.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Wenger amesema huenda akauanza msimu pasipokua na baadhi ya wachezaji wake ambao bado ni majeruhi.

Arsène Wenger ambae bado ana deni huko Emitarates la kuhakikisha anatwaa ubingwa wa michuano yoyote atakayoshiriki msimu huu amezungumza suala hilo huku akitarajia kuwakabili Liverpool siku ya Jumapili kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi.

Amesema baadhi ya wachezaji wake walitarajiwa kufanyiwa vipimo hii leo ama kesho kwa lengo la kufahamika kama ataweza kuwatumia katika mchezo huo lakini baadhi yao hawatokuwepo kabisa.

Wachezaji waliotarajiwa kufanyiwa vipimo ni Denilson mwenye maumivu ya misuli ya tumbo pamoja na Abou Diaby anaesumbuliwa na kiazi cha mguu huku Johan Djourou, Nicklas Bendtner, Alex Song pamoja na Aaron Ramsey wakiwa majeruhi.

Hata hivyo mzee huyo wa kifaransa amesema bado hajafahamu kama ataweza kuwatumia ama kutowatumia Robin van Persie ama Cesc Fabregas baada ya kuchelewa kuripoti mazoezi kufuatia kuwa na mapumziko ya kipindi cha majuma matatu mara baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment