KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 27, 2010

GAUCHO AMUHITAJI ZLATAN.


Ronaldo de Assis Moreira (Ronaldinho Gaúcho) ameueleza uongozi wa klabu ya AC Milan, atakuwa mwenye furaha zaidi endapo utafanikisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Sweden na klabu ya Barcelona Zlatan Ibrahimovic.

Ronaldinho Gaúcho ameyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya uongozi wa klabu ya AC Milan kuonekana kuwa atayri kujiingiza katika mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umroi wa miaka 28.

Ronaldinho Gaúcho, mwenye umri wa miaka 30, amesema endapo Zlatan Ibrahimovic atajiung na AC Milan kutakuwepo kwa ukomavu wa kikosi chao msimu huu.

Zlatan Ibrahimovic kabla hajajiunga na klabu ya Barcelona alikua akiichezea klabu ya Inter Milan ambayo ni hasimu mkubwa wa AC Milan huko nchini Italia.

No comments:

Post a Comment