KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

Javier Mascherano AMGOMEA MENEJA WAKE.


Mazingira ya usajili toka nchini Uinbgereza hadi katika kwenye klabu ya Barcelona, yalikua sababu tosha ya kumfanya kiungo wa kimataifa toka nchini Argentina Javier Mascherano kutojumuishwa kikosini usiku wa kuamkia hii leo pale Liverpool walipowatembelea Man City huko City of Manchester.

Sababu kubwa ya kiungo huyo kutojumuishwa kikosini imeelezwa kusababishwa na yeye binafsi baada ya kumuomba meneja wake asimpange hatua inayodaiwa huenda inalenga shinikizo la kuutaka uongozi wa klabu ya Liverpool umuuze huko kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona ambao wameshatangaza kutenga kiasi cha paund million 16 kama ada ya uhamisho wake lakini hata hivyo dau hilo halitoshi kufuatia Liverpool kuhitaji kiasi cha paund million 25.

Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson mara baada ya mchezo wa jana alilizungumzia suala hilo huku akidai kwamba bado anaamini Javier Mascherano ataendelea kusalia kwenye himaya yake.

Katika mchezo huo wa jana Man City walifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri yaliyofungwa na Gareth Barry 13 pamoja na Carlos Tévez 52 na 67.

Roberto Mancini meneja wa klabu ya Man City alionekana ni mwenye furaha alipozungumza na vyombo vya habari mara baada ya mtanange huo kumalizika huko City Of Manchester.

Alichosema ni kwamba amefurahishwa na ushindi huo wa kwanza katika ligi na anaamini huo ni mwanzo mzuri wa kuzibomoa timu nyingine.

Ushindi huo mkubwa wa Man city dhidi ya Liverpool ni kwanza toka mwaka 1937.

No comments:

Post a Comment