KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

NI KIONGOZI WETU KIKOSINI.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Urusi na klabu ya Arsenal Andrey Arshavin amesema kitendo cha nahodha na kiungo wao Cesc Fabregas kukubali kubaki Emirates anaamini kimewafurahisha wengi mbali na wachezaji wa klabu hiyo.

Andrey Arshavin amesema kila mmoja klabuni hapo alionekana kufurahishwa na hatua ya kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Hispania na anaamini kasi yao ya kuendelea kufanya vyema katika michezo inayowakabili kwa sasa inachangiwa na furaha iliopo.

Andrey Arshavin ameongeza kwamba licha ya kiungo huyo kuamua kubaki Emirates bado kuna mengi yanayoandikwa magazetini kila leo juu yake, na yeye binafsi amekua hayapi kipaumbele lakini kubwa anata itambulike kwamba Cesc Fabregas ni wa Arsenal nasi klabu nyingine.

No comments:

Post a Comment