KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 11, 2010

LUCA AJINASIBU KWA SASA NA BAADAE.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia Luka Modrić amesema anakiamini kikosi cha Spurs kitafanikiwa kuvuka katika hatua ya mchezo wa mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kuifunga klabu ya Young Boys ya nchini Uswiz.

Luka Modrić kiungo wa klabu hiyo ya jiji London amesema majukumu yao ni kuhakikisha wancheza kwa kujituma zaidi katika mchezo huo na kutimiza lengo la kutinga kwenye hatua ya makundi la michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 amesema kazi ya kuhakikisha wanatinga kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo itakua si ya kitoto hivyo itawalazimu kukaza buti na kuhakikisha wanaifunga klabu klabu ya Young Boys.

Wakati akijinasibu juu ya mpambano huo wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambao utachezwa kati kati ya juma lijalo, Luka Modrić amesema msimu huu huenda ukawa mgumu sana kwao kumaliza katika nafasi nne za juu katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza kama ilivyokua msimu uliopita.

Amesema kimtazamo wapinzani wao kama Liverpool pamoja na Man City wamejizatiti vilivyo kuhakikisha hawarejei makosa waliyoyafanya msimu uliopita.

Hata hivyo kiungo huyo bado akaendelea kusisitiza kwamba lengo lao ni kuendelea kuwepo hapo walipo ama kupanda juu zaidi hivyo watapigana kufa na kupona katika kuhakikisha wanasalia katika nafasi za juu.

No comments:

Post a Comment