KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

SHERIA ZAMKIMBIZA MMOJA BAADA YA MWINGINE.


Meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce amefanikiwa kumsajili beki wa kimataifa toka nchini uingereza Nedum Onuoha kwa mkopo wa muda mrefu.

Usajili wa beki huyo umefanywa ikiwa ni sehemu ya kutaka kuziba mwanya ulioachwa wazi na beki wa kimataifa toka nchini Ghana John Mensah aliekua huko Stadium of lights kwa mkopo misimu uliopita akitokea Olympic Lyon ya nchini Ufaransa.

Nedum Onuoha mwenye umri wa miaka 23 ameondoka Man city ikiwa ni sehemu ya kuendelea kupunguzwa kwa wachezaji wa klabu hiyo ambao wanatakiwa kusalia 25 kama sheria za ligi zinavyoelekeza.

Beki huyo anaondoka Manchester City baada ya kuichezea klabu hiyo miaka sita iliyopita ambapo mpaka anaondoka amecheza michezo 94 na kufunga mabao 3.

No comments:

Post a Comment