KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 20, 2010

NEYMAR AWAKATA MAINI CHELSEA.


Hatimae mshambuliaji wa pembeni wa kimataifa toka nchini Brazil Neymar da Silva Santos Júnior ametoa maamuzi ya kusalia nchini kwao na kuendelea kuichezea klabu ya Santos.

Neymar da Silva Santos Júnior ameyafanya maamuzi hayo usiku wa kuamkia hii leo na baada ya kitendo hicho uongozi wa klabu ya Santos ulimsainisha mkataba mpya wa miaka mitano.

Mkataba huyo aliyopewa Neymar da Silva Santos Júnior utamuwezesha kulipwa mshahara wa paund elfu 40 kwa juma sambamba na kuitaka klabu inayomuhitaji kwa sasa kumsajili kwa euro million 45 ambazo ni sawa na paund million 37.

Maamuzi ya Neymar da Silva Santos Júnior yanasitisha ndoto za klabu ya Chelsea kumsajili ambapo jana walitangaza kupandisha dau kutoka paund million 17 hadi 22 huku uongozi wa klabu ya Santos ulikua ukihirahi paund million 29.6.

No comments:

Post a Comment