KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 14, 2010

SAFARI YA WENGER YAONGEZEWA MUDA.


Safari ya meneja wa kimataifa toka nchini Ufaransa Arsene Wenger ya kusaka mafanikio huko Ashaburton Grove imeongezewa muda na uongozi wa klabu hiyo yanye maskani yake makuu kaskazini mwa jiji la London huko nchini Uingereza.

Safari ya babu huyo ya kuendelea kuwepo huko Emirates ilikua inaishia mwishoni mwa msimu huu na sasa itaendelea mpaka mwaka 2014.

Taarifa toka ndani ya uongozi wa klabu ya Arsenal zimedai kwamba meneja huyo ataendelea kuwepo klabuni hapo kama mkataba wake mpya unavyoeleza huku wakiwa na matumaini makubwa dhidi yake.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha taratibu za kusaini mkataba mpya Arsene Wenger mwenye umri wa miaka 60 amesema lengo lake ni kuendelea kusaka mafanikio akiwa na klabu hiyo aliyoanza kuifua toka mwaka 1996.

Mbali na kudai kuendelea kusaka mafanikio pia Arsene wenger amesema Arsenal tayari imeshaingia katika damu yake hivyo anahisi haoni sababu ya kuiacha klabu hiyo inayomuhitaji huku yeye akiihitaji pia.

Historia ya Arsene Wenger akiwa Arsenal yaonyesha kwamba tayari ameshaizawadia ubingwa wa ligi kuu klabu hiyo mara tatu ikiwa ni msimu wa mwaka 1997–98, 2001–02, 2003–04 kombe la FA mara (4) katika msimu wa mwaka 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05, ngao ya hisani (4): 1998, 1999, 2002, 2004 na kukifikisha hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa kikosi chake kabla ya kufunga na Barcelona mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment