KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

SEVILLA WAKUBAKI KUMUUZA Sebastien Squillaci.


Uongozi wa klabu ya Sevilla hatimae umekubali ofa ya klabu ya Arsenal iliyotumwa klabuni hapo mwishoni mwa juma lililopita kwa lengo la kusajiliwa kwa beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa Sebastien Squillaci.

Hatua ya kukubalia ofa hiyo imemfanya Sebastien Squillaci kufunga safari toka nchini Hispania usiku wa kuamkia hii leo na kuelekea jijini London nchini Uingereza tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na The Gunners.

Squillaci, mwenye umri wa miaka 30, anatarajia kujiunga na klabu ya Arsenal kwa lengo la kuziba pengo lililoachwa na mabeki wanne walioondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu uliopita.

Miongoni mwa mabeki hao ni William Gallas, Mikael Silvestre (Ufaransa) Sol Campbell ( Uingereza) pamoja na Philippe Senderos (Uswiz).

No comments:

Post a Comment