KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 23, 2010

RUNGU LA UEFA LAIANGUKIA FK Rabotnicki.


Shirikisho la kabumbu barani Ulaya UEFA limeiadhibu klabu ya FK Rabotnicki kwa kuitoza Euro 10,000 ambazo ni sawa na paund 8,000 kufuatia vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyoonyeshwa na mashabiki wa klabu hiyo wakati wa mchezo wa hatua ya mtoano dhidi ya Livepool mwezi uliopita.

Adhabu hiyo ya UEFA kwa klabu hiyo imetolewa baada ya kamati ya nidhamu kuketi chini na kufuatilia taarifa zilizowasilishwa mezani kwao na kubainika kwamba ni kweli mashabiki wa klabu hiyo walionyesha vitendo vya ubaguzi kwa baadhi ya wachezaji wa klabu ya Liverpool wenye asili ya bara la afrika.

Kamati hiyo pia imefuatilia picha za televisheni ambazo zimeonyesha mashabiki hao walivyokua wakilia kama Sokwe mtu wakati kinda wa Liverpool David Amoo alipokua akigusa mpira.

Mbali na David Amoo pia David Ngog aliefunga mabao mawili pekee yake katika mchezo huo alikumbwa na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment