KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 26, 2010

USAJILI WA ROBINHO KIZUNGUMKUTI.


Ndoto za kiungo mshambuliaji wa klabu ya Man City Róbson de Souza Robinho za kutaka kuelekea nchini Hispania ama Italia bado zipo katika hali ya sintofahamu kufuatia mkanganyiko wa taarifa za uhamisho zinazoelndelea kujitokeza.

Ndoto za mchezaji huyo zimeendelea kutia mashaka kufuatia taarifa zilizotolewa na vyombo mbali mbali vya habari zinazodai kwamba mchezaji huyo huenda akatumika kama sehemu ya kubadilishana na Zlatan Ibrahimavic wa klabu ya Barcelona ama kusajiliwa na klabu ya Ac Milan ya nchini Italia.

Hatua ya kubadilishana wachezaji hao imekuja kufuatia uongozi wa klabu ya Man city kumuhitaji mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Sweden Zlatan Ibrahimavic ili hali Fc Barcelona wakimuhitaji kwa udi na uvumba Róbson de Souza Robinho.

Hata hivyo dili hilo, limejitokeza baada ya taarifa kueleza kwamba uongozi wa klabu ya AC Milan ulikuwa unajipanga kufanya mazungumzo ya kumsajili Zlatan Ibrahimavic toka Barcelona na muda mchache baadae Man city waliingilia kati.

Alipoulizwa meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini juu ya suala hilo alijibu bado suala la mchezaji huyo lina muda wa siku sita hivyo wanampa uhuru wa kuchagua kama anataka kurejea Hispania ama kuanza maisha mapya huko nchini Italia.

Roberto Mancini amesema licha ya Robinho kutarajia kuondoka huko Eastland bado ana mahusiano mazuri na mchezaji huyo na kila leo amekua akimtaka kufanya maamuzi yaliayo sahihi ya kucheza soka lake.

No comments:

Post a Comment