KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 18, 2010

Amos Adamu NA MWENZAKE KIKAANGONI.


Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA inatazamia kutangaza hukumu ya wajumbe wa kamati kuu ya shirikisho hilo ambao walijishughulisha na suala la rushwa wakati wa kipindi hiki cha kuelekea kupiigia kura nchi itakayoandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 pamoja na 2022.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa kwa Amos Adamu mjumbe kutoka nchini Nigeria pamoja na Reynald Temarii mjumbe kutoka Tahiti ambao kwa sasa wamesimamishwa na shirikisho hilo kwa lengo la kupisha upelelezi uchukue mkondo wake baada ya gazeti Sunday Times la nchini Uingereza kuchapisha habari zinazohusiana na wajumbe hao kuomba rushwa.

Hata hivyo wakati upelelezi ukiendelea na ukitarajiwa kufikia ukingoni hali ni mbaya kwa wajumbe hao kufuatia ushahidi unaoendelea kujidhirisha wazi kwamba waliomba rushwa kwa moja ya nchi zinazoomba nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia ili waweze kuipigia kura na kuzitosa nchi nyingine.

Kwa upande wa Amos Adamu ushahidi wa gazeti la Sunday Times la nchini Uingereza umeonyesha kuwa aliomba pesa za ujenzi wa viwanja zipitie kwenye akaunti ambazo zina majina na watoto wake.

Na kwa upande wa Reynald Temarii ushahidi wake waonyesha kuwa aliomba fedha kwa kisingizio cha kuimarisha vifaa vya michezo nchini Tahiti bila ya yeye kupata faida yoyote.

Endapo kamati ya nidhamu ya FIFA itatoa adhabu kwa wajumbe hao, nafasi zao za kupiga kura Disemba mbili zitafutwa na shisrikisho hilo litaitisha mkutano wa kuwachagua wajumbe wengine wa kamati kuu mwezi Februari mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment