
Wakati Liverpool wakiendelea kusaka dawa ya kurudi kwenye mfumo wa ushindi, hali inaonekana kuwa mbaya zaidi ndani ya klabu hiyo kufuatia wachezaji muhimu kuumia kila kukicha.
Klabu hiyo ambayo inasuasua katika utaratibu wa kusaka ushindi mwishoni mwa juma lililopita ilimpoteza mshambuliaji wake wa kutumainiwa Ferdnando Torres ambae anasumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu na sasa nahodha na kiungo muhimu Steven Gerrard ameungana na mshambuliaji huyo katika benchi la wachezaji majeruhi.
Steven Gerrard amelazimika kukalia benchi hilo baada ya kuumia kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo kati ya nchi yake ya Uingereza dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa hatua ambayo imeonekana kuwakera mno mashabiki wa klabu ya Liverpool.
Steven Gerrard ameumia nyonga na huenda ikamchukua muda mrefu kurejea tena katika hali yake ya kawaida hali ambayo imeongeza hofu kwa masjhabiki hao ambao wana hamu ya kuiona Liverpool ikirejea katika makali yake.
No comments:
Post a Comment