
Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti ameendelea kushikilia msimamo wake wa kusifia mfumo wa uchezaji wa kikosi chake licha ya kupata point moja katika michezo mitatu ya ligi iliyopita.
Carlo Ancelotti ameendelea na msimamo huo huku mashabiki wengi wa klabu ya Chelsea wakionekana kukatishwa tamaa na mikakati anayoitumia toka wapopoteza mchezo dhidi ya Sundeeland walioibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri huko Stamforde Bridge.
Akizungumzia mchezo wa jana dhidi ya Newcastle uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja, meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia amesema wachezaji wake kwa ujumla walionyesha kiwango kizuri na kilichowaangusha ni bao la mapema lililofungwana wapinzani wao kwa mpira uliorejeshwa kwa bahati mbaya na beki wake wa kimataifa toka nchini Brazil Alex.
Amesema mpira uliopigwa na beki huyo ulionyesha kulikua hakuna mawasiluiano mazuri kati yake na kipa Peter Cech hatua mbayo ilimpa mwanya mshambuliaji wa Newcastle utd Andy Carrol kupachika bao la kuongoza.
Hata hivyo Carlo Ancelotti amekiri kuwa na kazi ya ziada ya kuhakikisha kikosi chake kinacheza vizuri zaidi na kufikia hatua ya kupata ushindi kama ilivyokua mwanzoni mwa msimu huu ambapo walianza vyema na kufanikiwa kuongoza ligi hadi mwishoni mwa juma lililopita.
Katika hatua nyingine Carlo Anceloti amezungumzia kurejea kwa nahodha na beki wa kikosi chake John terry ambapo amesema kesho anatarajia kuanza mazoezi sambamba na wachezaji wenzake huku kiungo Frank Lampard akimtarajia kurejea tena uwnajani juma lijalo hususan katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Olympique Marseille.
No comments:
Post a Comment