KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, November 29, 2010

Jamie Carragher ATEUKA BEGA.


Nahodha msaidizi pamoja na beki wa klabu ya Liverpool Jamie Carragher itamchukua muda wa mwezi mmoja kurejea tena uwanjani baada ya kuteuka bega lake la kushoto alipokua kwenye mchezo wa jana dhidi ya Spurs.

Imefahamika kuwa Jamie Carragher atakua nje kwa muda huo baada ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimetoa nafasi kwa daktari wa klabu ya Liverpool kumtaka beki huyo kuwa nje kwa ajili ya matibabu.

Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson alieonyesha wasi wasi wake juu ya mchezaji huyo toka jana mara baada ya mchezo dhidi ya Spurs ambapo alikaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba Jamie Carragher huenda ikamchukua muda mrefu kupona jeraha linalomkabili hatua ambayo imethibitika mara baada ya vipimo kutolewa.

Hata hivyo mara baada ya vipimo kutoka meneja huyo ameonyesha hali ya huzuni huku akisikitika kwa utaratibu uliopo ambao amekiri unamfanya aendelee kuwakosa wachezaji muhimu kama Steven Gerrard pamoaj na Daniel Agger ambao wanajiunga na Jamie Carragher ambae jana alikua akiitumikia Liverpool katika mchezo wa 450.

Mzee huyo wa kiingereza pia akaonyesha hali ya kusikitishwa na matokeo aliyoyapata jana kwenye uwanja wa White Hert Lane ambayo yanaendelea kukiweka njia panda kikosi chake ambacho kimeweka malengo ya kurejea katika nafasi nne za juu msimu huu.

No comments:

Post a Comment