
Shirikisho la soka dunaini FIFA linatarajia kutoa kauli juu ya matatizo yanayoendelea ndani ya chama cha soka nchini Zambia FAZ pamoja na ndani ya chama cha soka nchini Ghana GFA.
FIFA wanatarajia kutoa kauli hiyo kufuatia matatizo yaliyojitokeza ndani ya vyama hivyo huku ikisemekama serikali za nchi hizo mbili zimepenyeza mikono ya madaraka na kutaka kupindua sheria zilizowekwa kwa misingi ya kuendesha mchezo wa soka.
Wajumbe wa ngazi za juu wa FIFA wanatarajiwa kuelekea nchini Zambia kwenda kuchunguza chanzo cha zogo linaloendelea kati ya wajumbe wa chama cha soka nchini humo dhidi ya mwenyekiti Kalusha Bwalya ambae anadaiwa kwenda kinyume na taratibu za soka zinavyoagiza.
Utaratibu huo unadaiwa kumpa nafasi kila mmoja ambae hakubaliani na utawala wa Bwalya kumpinga kiongozi huo huku ikisemekana hadi viongozi wa serikali ya nchi hiyo wamekua wakiungana na wadau wa soka kumshinikiza kiongozi huyo wa ngazi za juu aachie madaraka.
Kubwa linalodaiwa kwa kiongozi huyo wa soka nchini Zambia ambae pia alishawahi kuichezea timu ya taifa ya Zambia, ni kuzidisha muda wake wa uongozi na kuzuia kipindi cha uchaguzi ambacho kilitakiwa kuchukua mkondo wake ndani ya miezi kadhaa iliyopita.
Nchini Ghana wajumbe hao wa FIFA napo watakwenda kufanya uchunguzi kufuatia sakata la viongozi wa serikali kukitaka cha cha soka nchini humo kulipitisha jina la nahodha na mchezaji wa zamani wa Black Stars Abeid Pele ambae anapigiwa chepuo la kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Hatua hiyo ya serikali ya nchini Ghana imeshapingwa vikali na viongozi wa chama cha soka nchini humo ambao tayari wameshalipitisha jina na mwenyekiti wao Kwesi Nyantakyi kuwania nafasi ya ujumbe wa CAF.
Matatizo kama hayo ya serikali kuingilia mfumo wa uendeshaji soka tayari yameshazikumba nchi kama Nigeria, Chad, Niger pamoja na Kenya ambazo zilikumbwa na adhabnu ya kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment