KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, November 29, 2010

HOFU YATANDA SPURS.


Meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp ameonyesha wasi wasi juu ya hali ya kiungo wake wa kimataifa toka nchini Uholanzi Rafael van der Vaart ambae alipata maumivu ya nyama za paja alipokua kwenye mchezo wa jana dhidi ya Liverpool.

Harry Redknapp amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 hii leo alitarajiwa kufanyiwa vipimo ambavyo vitatoa picha kamili ya ukubwa wa jeraha linalomkabili ambalo pia analihofia huenda likamuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kijacho.

Amesema kuumia kwa Rafael van der Vaart kunampa wakati mgumu wa kubuni mfumo mpya ndani ya kikosi chake ambacho mara kadhaa kimekua kikimtegemea kiungo huyo ambae mpaka sasa ameshaifungia Spurs mabao 11 katika michezo 21 aliyocheza.

Harry Redknapp pia amezungumzia hali ya beki wake wa kimataifa toka nchini Ufaransa Younes Kaboul ambae pia alipata maumivu ya Hips alipokua kwenye mchezo wa jana dhidi ya Liverpool waliokubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 24 hali yake sio mbaya sana lakini pia nae alitarajiwa kufanyiwa vipimo hii leo.

Hata hivyo amedai kuumia kwa Younes Kaboul sio tatizo kubwa sana ndani ya kikosi chake, kwani anamtarajia beki wa kiingereza Michael Dawson kurejea uwanjani wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Katika hatua nyingine Harry Redknapp amewasifia wachezaji wake kwa soka safi la kiushindani walilolionyesha katika mchezo wa jana dhidi ya Liverpool ambao walipata nafasi ya kuongoza kwa idadi ya bao moja kwa sifuri lililofungwa na Mikael Škrtel katika dakika ya 42 kabla beki huyo wa kimataifa toka nchini Slovakia hajajifunga mwenyewe katika dakika ya 65 kupitia mpira uliopigwa na Luca Modric na kisha Aron Lenon kuongeza bao la pili katika dakika dakika za lala salama .

Amesema kwa kipindi chote kikosi chake kilionyesha hali ya kuwa na njaa ya kusaka ushidni na hatua hiyo ilijidhighirisha kabla ya filimbi ya mwisho haijapulizwa.

Ushindi wa mabao mawili kwa moja umeifanya spurs kufikisha idadi ya point 25 ambazo zinaifanya klabu hiyo ya London kukwea kwa nafasi moja kutoka nafasi ya sita hadi ya tano.

No comments:

Post a Comment