KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, November 22, 2010

GALLAS KUENDELEA KULA BATA SPURS.


Beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa William Gallas ameendelea kupewa heshima ya kuwa nahodha wa kikosi cha Tottenham baada ya kukiongoza kikosi hicho kupata ushindi wake wa kwanza kwa kuifunga klabu ya Arsenal nyumbani kwa kipindi cha miaka 17.

Gallas amepewa heshima hiyo baada ya kukaimu nafasi ya unahodha ambayo hushikiliwa na Ledley King kwa kusaidiana na wasaidizi wake ni akina Luka Modric, Michael Dawson pamoja na Tom Huddlestone ambao wote kwa pamoja ni majeruhi.

Meneja wa klabu ya tottenham Harry Redknapp amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 33 ataendelea kushika nafasi hiyo hadi wahusika watakaporejea katika hali zao na kuanza kucheza katika kikosi cha kwanza.

Amesema anamuamini Gallas katika utaratibu wa kukiongoza kikosi chake hivyo hana shaka na suala hilo ambalo pia limeonekana kubarikiwa na wachezaji wengine klabuni hapo.

Baraka hizo zinamfanya Willium Gallas kukiongoza kikosi cha Spurs kwa mara nyingine tena siku ya jumatano kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo Tottenham watakuw anyumbani kwa kuwakaribisha Weder Bremen toka nchini ujerumani.

No comments:

Post a Comment