
Beki na nahodha msaidizi wa klabu ya Man City Kolo Toure amewataka viongozi wa klabu hiyo kuwa wakali kwa baadhi ya wachezaji ambao amedai hawajitumui ipasavyo wanapokua uwanjani katika harakati ya kuzisaka point tatu muhimu.
Toure aliesajiliwa na klabu y hiyo ya mjini Manchester akitokea Arsenal mwaka 2009, ametoa rai hiyo kwa viongozi baada ya kuonyesha kuchoshwa na baadhi ya wachezaji wenzake ambao amedai wanawaangusha kila kukicha.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema mbali na viongozi kutengeneza mfumo wa kuwa wakali pia kuna ulazima kwa wachezaji wasiojituma kukatwa mishahara yao ili iwe sehemu ya kuongeza changamnoto ya kujituma na kufikia malengo ya ushindi unaohitajika kila wanapoingia uwanjani.
Amesema yu tayari kuwataja wachezaji ambao hawajitumi na hii itakua kwa nia safi na wala si kwa nia ya kuharibu.
Hata hivyo Kolo Toure ameutaka uoingozi kufanya hivyo huku ikiaminika kwamba ndugu yake Yaya Toure ambae alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea FC Barcelona ndie analipwa kiasi kikubwa cha fedha kama mshahara huku ikidai analipwa paund laki mbili kwa juma.
Kabla ya ushindi wa jana Man city walikua wakisuasua katika michezo ya ligi kuu kufuatia matokeo ya sare yaliyokiandama kikosi hicho cha Bilionea wa kiarabu Sheikh Mansour ambae alitoa kiasi cha paund milion 120 kwa ajili ya kufanya usajili wa msimu huu.
No comments:
Post a Comment