KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, November 30, 2010

GHANA WASAKA KOCHA WA BLACK STARS.


Beki na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Marcel Desailly amekua mmoja wa makocha wanaowaniwa na chama cha soka nchini Ghana ambacho kipo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchini hiyo Black Stars.

Chama cha soka nchini Ghana kimethibitisha kuwepo kwa jina na gwiji huyo aliewahi kuvichezea vilabu nguli huko barani Ulaya, baada ya kutangaza majina matano ya makocha waliosalia kufuatia mchujo uliofanywa jana.

Mbali na Marcel Desailly, majina mengi yaliyosalia katika orodha ya kinyang’anyiro hicho ni jina la kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco Humberto Cuelho, meneja wa zamani wa klabu ya Partizan Belgrade ya nchini Serbia Goran Stevanovic, kocha wa kituruki Can Vanli pamoja na Herbert Addo anaekinoa kikosi cha Ghana kwa sasa.

Ghana wapo katika mchakato huo baada ya kumalizana na aliekua kocha wa Black Stars Milovan Rajevac kutoka nchini Serbia ambapo hata hivyo kocha huyo alionyesha dhamira ya kutaka kurejea tena katika madaraka yake lakini viongozi wa chama cha soka nchini Ghana hawakumpa kipaumbele.

Wasifu wa makocha hao watano waliosalia katika kinyang’anyiro hicho kwa upande wa Desailly, yeye ni Mfaransa aliezaliwa nchini Ghana katika jiji la Accra, alikua mmoja wa wachezaji walioiwezesha Ufaransa kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998 huku klabu alizozitumikia ni Olympique Marseille, AC Milan pamoja na Chelsea.

Cuelho ameshawahi kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Ureno na kufanikiwa kufika kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya fainali za mataifa ya bara la Ulaya mwaka 2004, huku wasifu wake mwingine ni kuwahi kukifundisha kikosi cha timu ya taifa ya Morocco pamoja na Tunisia.

Goran Stevanovic, yeye alishawahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Serbia na mchango wake uliifikisha nchi hiyo kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2006 na kisha akaizawadia ubingwa wa ligi ya nchini Serbia klabu ya Partizan Belgrade.

Herbert Addo alikua kocha wa klabu ya Aduana Stars ambayo aliiwezesha kumaliza katika nafasi ya kwanza msimu uliopita na sasa anakinoa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana huku akikiongoza kikosi cha taifa hilo cha wachezaji wa ndani kufuzu kucheza fainali za mataifa bingwa barani Afrika CHAN.

No comments:

Post a Comment