
Wakati FIFA wakionyesha kuchukizwa na suala la rushwa, sakata lingine la rushwa limeibuliwa huku wajumbe watatu wa kamati kuu ya shirikisho hilo ambao wanatarajia kupiga kura ya kuzichagua nchi zitakazoandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 pamoja na 2022 wakihusika.
Sakata hilo limeibuliwa na kipindi cha Panorama ambacho hurushwa na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC ambapo imebainika Nicolas Leoz, Issa Hayatou pamoaj na Ricardo Teixeira walihusika kuchukua mlungula mwaka 1995.
Hata hivyo FIFA wameonyesha kutokua tayari kulizungumzia sakata hilo huku madai yao yakilenga kujiandaa na zoezi la upigaji wa kura wa kuzichagua nchi zitakazoandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 pamoja na and 2022 litakalofanyika mjini Zurich nchini Uswiz Desemba 2 mwaka huu.
Nchi zinazowania nafasi hiyo ya kuwa mwenyeji ni Uingereza Urusi, Hispania kwa kushirikiana na Ureno pamoja na Uholanzi kwa kushirikiana na Ubelgiji.
Kwa upande wan chi zinazowania kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 2022 ni Australia, Japan, Qatar, Korea Kusini pamoja na Marekani.
No comments:
Post a Comment