
Wakati siku 32 zikiwa zimesalia kabla ya dirisha dogo la usajili halijafunguliwa uongozi wa klabu ya Sevilla umetangaza nia ya kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya Liverpool Lucas Leiva.
Taarifa toka ndani ya uongozi wa klabu hiyo zimeeleza kuwa Lucas Leiva ameingia katika orodha ya kusajiliwa klabuni hapo mwezi januari kufuatia uwezo wake kuonekana unafaa kuibeka Sevilla ambayo kwa sasa imempoteza kiungo wake wa kimataifa toka nchini Italia Tiberio Guarente alie majeruhi.
Kabla ya kufikiria kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, uongozi wa klabu ya Sevilla tayari ulikua umeshajipanga kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Denmark Christian Poulsen mwanzoni mwa mwezi huu, lakini maamuzi hayo yaligeuka baada ya Lucas kuonyesha mvuto zaidi wa kiuchezaji.
No comments:
Post a Comment