
Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspur Niko Kranjcar amesema yu tayari kuondoka klabuni hapo wakati wowote kuanzia sasa.
Niko Kranjcar kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia ametamsimo huo baada ya kuchukizwa na kitendo cha kendelea kuwekwa benchi licha ya uwezo wake kufahamika na meneja wa klabu hiyo Harry Redknapp.
Kiungo huyo aliejiunga na Spurs mwaka 2009 akitokea kwenye klabu ya Portsmouth amebainisha hadharani kwamba toka aliposajiliwa kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Rafael van der Vaart mchango wake umekua hauthaminiki hivyo anaona ni bora atafute mahala pengine ambapo atawezeshwa kucheza kila juma.
No comments:
Post a Comment