
Wachezaji wa kikosi cha klabu ya Arsenal wametakiwa kusahau matokeo mabovu yaliyopatikana mwishoni mwa juma lililopita ya kuchapwa mabao matatu kwa mawili na mahasimu wao wakubwa Tottenham Hotspurs, na kufikiria mchezo ujao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya fc Bargha ya nchini Ureno.
Rai hiyo kwa wachezaji imetolewa na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Morocco Marouane Chamakh ambapo amesema kilichotokea katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ni matokeo ya soka hivyo hakuna sababu ya kuendelea kukipa nafasi katika vichwa vyao.
Amesema anaamini kila mmoja klabuni hapo anaumizwa na hatua ya kufungwa na Spurs ili hali walikua wakiongoza kwa idadi ya mabao mawili kwa sifuri, lakini ukweli ni kwamba hawana budi kusahau na kufikiria lililo mbele yao.
Amesema mchezo ulio mbele yao ni muhimu zaidi ya matokeo yaliyopatikana kutokana na kuwa katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Arsenal wanakwenda mjini Braga nchini Ureno kupambana na wenyeji wao, huku wakichagizwa na ushindi wa mabao sita kwa sifuri walioupata kwenye mchezo wa awali wa kundi H uliozikutanisha klabu hiyo kwenye uwanja wa Emirates.
Katika hatua nyingine gwiji wa soka nchini Uingereza Ian Wright ametoa ushauri kwa meneja wa kikosi cha klabu ya Arsenal Arsene Wenger kwa kumtaka akiboreshe kikosi chake kitakapofika kipindi cha usajili mwezi januari mwaka 2011.
Ian Wright ambae aliwika na klabu ya Arsenal kuanzia mwaka 1991–1998 na kuifanikia kufunga mabao 128 kwenye michezo 221 aliyocheza ameongeza kuwa kikosi kilichopo sasa cha klabu hiyo sio kibaya bali kinahitaji usaidizi wa wachezaji ambao wataleta changamoto mpya.
No comments:
Post a Comment