
Uongozi wa klabu ya Chelsea umekanusha taarifa za meneja wao Carlo Ancelotti yu mbioni kuachia nagazi kufuatia matokeo mabovu yaliyokiandama kikosi chake kwa kipindi cha majuma mawili mfululizo.
Uongozi wa klabu hiyo umelazimika kukanusha taarifa hizo baada ya baadhi ya vyombo vya habari mapema hii leo kuripoti meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia yu tayari kuachia ngazi mara baada ya kuona mambo hayamuendei vizuri klabuni hapo.
Uvumi wa kuondoka kwa Ancelotti ulianza kuzungumzwa katika vyombo vya habari mara baada ya kauli yake aliyoizungumza ambayo ilieleza kwamba hastahili kufananishwa na meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson, kwa mazuri aliyoyafanya na hii inatokana na meneja huyo kuwa na mipango mizuri ndani ya kikosi chake.
Kauli hiyo ya Anceloti imechukuliwa kama tusi kwa uongozi wa klabu ya Chelsea ambao mpaka hii leo umeshindwa kupanga mikakati mizuri ambayo inashindwa kuwafikia Man Utd.
Carlo Ancelotti akaendelea kumwaga mchele kwa kusema uongozi wa klabu ya Chelsea umekua haumshirikishi katika maamuzi unayoyafanya hivyo haoni sababu ya kuendelea kuwa sehemu ya klabu hiyo ambayo mara nyingi maamuzi yamekua yakitoka moja kwa moja kwenye ngazi ya juu.
Akizungumzia suala la kuondoka kwa aliekua msaidizi wake Ray Wilkins na kuteuliwa mbadala wake, mtaliano huyo amesema hakushirikishwa hata kidogo bali alichosiakia msaidizi wake anaondoka kwa sababu za mkataba wake kufikia kikomo na juma moja baadae aliteuliwa Michael Emenalo kuwa meneja msaidizi.
Hata hivyo mwishoni mwa juma hili Carlo Anceloti aliulizwa juu ya kuondoka kwa Ray Wilkins na alijibu hafahamu lolote zaidi ya kujua maamuzi hayo yalitoka kwa uongozi wa juu.
No comments:
Post a Comment