
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez ameushangaza uongozi wa klabu ya Manchester City, baada ya kuundikia barua ya kutaka aruhusiwe kuondoka klabuni hapo.
Tevez mwenye umri wa miaka 26 inasemekana ameandika barua hiyo baada ya kuchukizwa na baadhi ya taratibu za huko Estaland ambazo mara kadhaa zimekua zikimfanya achukizane na meneja wake Roberto Mancini.
Mbali na kuchukizwa na taratibu hizo, pia mshambuliaji huyo inasemaka amekuwa akitamani sana maisha ya nyumbani kwao Argentina baada ya kuchoshwa na maisha ya Uingereza ambapo mpaka sasa ameishi nchini humo kwa miaka minne.
No comments:
Post a Comment