KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 11, 2010

MAN UTD Vs ARSENAL


Homa ya pambano la jumatatu kati ya Man Utd dhidi ya Arsenal imeendelea kupanda, ambapo baada ya jana meneja wa Mashetani wekundu Sir Alex Ferguson kulonga kupitia Michezo na Times hii leo meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anazungumzia upande wa kikosi chake.

Arsene Wenger ambae siku ya jumatatu ataifunga safari ya kuelekea Old Trafford kusaka point tatu muhimu amesema kikosi chake kipo kamili kwa ajili ya mchezo dhdi ya Man Utd ambao wanakwenda kukutana nao wakiwa na rekodi nzuri ya kutokufungwa mchezo hata mmoja wa ligi msimu huu.

Amesema kikosi chake kwa msimu huu kimekua na rekodi nzuri kinapocheza nje ya uwanja wa nyumbani licha ya kurekebisha makosa madogo madogo yalipelekea kupoteza kiasi kikubwa cha michezo ya nyumbani hivyo anaamini kasumba hiyo itaendelezwa hadi katika mchezo huo wa mwanzoni mwa juma lijalo.

Mzee huyo wa kifaransa pia amezunguimzia ratiba ya ligi ambapo ameeleza wazi kwamba mwezi huu kwao utakua mzuri kutokana na michezo inayowakabili ambayo anaamini itakipa changamoto kikosi chake kusaka namna ya kupata point tatu muhimu.

Katika hatua nyingine Arsene Wenger ameonyesha heshima kwa hatua iliyofikiwa na meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson ya kudumu na klabu ya hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka 20 hali ambayo inamfanya kuwa meneja wa kipekee kwenye soka la nchini Uingereza.

Mzee huyo pia akajizungumzia yeye binafsi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 aliyopita ambayo imeshuhudia akiwa na klabu ya Arsenal ambayo inasimama badala ya jina lake pale unapofika wakati kama huu wa kushindana na Man Utd ambayo nayo inasimama badala ya jina la Sir Alex Ferguson.

No comments:

Post a Comment