KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 1, 2010

David Gold AONGEZA MATUMAINI KWA MYAHUDI.


Mmiliki mwenza wa klabu ya West ham Utd David Gold amesema mwenendo wa ushindi unaoendelea katika kikosi cha klabu hiyo unampa nafasi ya kuanza kuamini wanaweza kuondoka kwenye ukanda wa kushuka daraja msimu huu.

David Gold amesema licha ya kuanza kuamini huko bado ana imani na meneja wakiyahudi Avram Grant kuwa anaweza kuifanya kazi hiyo na kufikia hatua ya kupanda hadi kwenye nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Amesema kazi kubwa iliopo sasa ni kuhakikisha West Ham Utd inaondokana na kasumba ya kumaliza ligi ikiwa katika nafasi za chini kama ilivyokua msimu uliopita ambapo meneja wa kitaliano Gianfranco Zola alijitahidi kuhakikisha klabu hiyo ya London haishuki na mwisho wa msimu alifanikiwa baada ya kujikusanyia point 35 ambapo hata hivyo walimtimua kazi.

Hata hivyo David Gold amekiri kazi iliopo ni kubwa lakini bado akaendelea kusisitiza kuwa na imani na Avram Grant anaweza kazi ya kuinusuru West ham utd ambayo usiku wa kuamkia hii leo ilifanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kuibanjua Man Utd mabao manne kwa sifuri.

No comments:

Post a Comment