



Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema hakuna sababu yoyote ya kumuharakisha nahodha na kiungo wake Cesc Fabregas kurejea uwanjani kwa uharakla kama baadhi ya mashabiki wengi wanavyohitaji.
Wenger amekata ngebe hizo za baadhi ya mashabiki huku akiwataka watambue kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Hispania haifahamiki atarejea uwanjani lini, nah ii ni kutokana na ukubwa wa jeraha linalomsumbua toka kati kati ya juma lililopita alipokua kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Braga.
Mzee huyo wa kifaransa amelazimika kulitolea ufafanuzi jambo hilo alipoulizwa na waandishi wa habari, usiku wa kuamkia hii leo muda mchache baada ya mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya arsenal na Wigan Kumalizika huko Emirates Stadium.
Amesema yeye yupo tayari kumsubiri mchezaji huyo hadi atakapopoa kabisa jeraha la nyama za paja linalomsumbua na anaona hiyo itakua njia sahihi ya kumtumia vyema kwenye kikosi chake ambacho msimu huu kimepania kutwaa moja ya ubingwa wa michuano wanayoshiriki.
Akizungumzia mchezo wa jana ambao ulimalizika kwa vijana wake kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya Wigan, Arsene Wenger amewapa tano wachezaji wake kwa mchezo mzuri waliouonyesha na kufikia hatua ya kutimiza lengo la kusalia kwenye michuano hiyo ya kombe la ligi ambayo inaelekea katika hatua ya nusu fainali.
Amesema msimu huu kikosi chake kimepoteza michezo mingi nyumbani zaidi ya ugenini, hivyo ushindi wa jana ana imani utakua umewapa changamoto wachezaji wake kujiamini zaidi pindi watakapokutana na Fulham mwishoni mwa juma hili.
No comments:
Post a Comment