KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 1, 2010

GHANA YAPEWA ONYO KALI.


Shirikisho la soka duniani FIFA limeionya serikali ya nchini Ghana kuacha kabisa utaratibu wa kuingilia masuala la soka ya nchi hiyo na kama itaendelea nchi hiyo itafungiwa kushiriki michunao ya kimataifa.

Onyo hilo kwa serikali ya nchini Ghana limetolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na shirikisho hilo la soka duniani kote ambapo imebainika kuwa viongozi wa serikali ya nchini Ghana wamekua na kasumba ya kuushurutisha uongozi wa chama cha soka kufanya kinachotakiwa na serikali hatua ambayo ni kinyume na taratibu za soka.

Uchunguzi uliofanywa na FIFA umetokana na kitendo cha serikali ya nchini Ghana kuushurutisha uongozi wa chama cha soka nchini humo kupitisha jina la nahodha na mchezaji wa zamani wa Black Stars Abedi Pele kwa lengo la kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF, ombi ambalo lilipingwa vikali na viongozi wa chama hicho GFA.

Ombi hilo lilipingwa baada ya viongozi wa GFA, kukubaliana kwa pamoja kulipitisha jina na mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Kwesi Nyantakyi kuwania nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati kuu ya CAF hali ambayo ilionekana kuwakera mno viongozi wa serikali.

Endapo serikali ya nchini Ghana itarejea tena kuingilia kati masuala la soka, huenda nchi hiyo ikafungiwa na FIFA kama ilivyokua kwa nchi za Nigeria, Chad, Niger pamoja na Kenya.

No comments:

Post a Comment