
Shiriksiho la soka barani Ulaya UEFA limemuadhibu meneja mkuu wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho kwa kumtaka asikae kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo katika michezo miwili baada ya kumkuta na hatia ya kuwa chanzo cha wachezaji wake kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Ajax Amsterdam uliochezwa juma lililopita huko nchini Uholanzi.
UEFA wametangaza kumfungia meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno sambamba na kumtoza fainali ya Euro 120,000 ambazo ni sawa na paund za kiingereza 100,305.
UEFA pia imewaadhibu wachezaji wanne waliohusika na tuhuma hiyo kwa kuwatoza faini ya Euro, 40,000 ambazo ni sawa na paund za kiingereza 33,434 ambapo wachezaji hao ni Xabi Alonso, Sergio Ramos, Iker Casillas pamoja na Jerzy Dudek.
Maamuzi ya UEFA yametolewa baada ya uthibitisho kupatikana kupitia picha za televisheni ambazo zimemuonyesha Mourinho akimtuma Xavi Alonso afanye kosa la makusudi kwa lengo la kuonyeshwa kadi nyekundu, huku picha hizo pia zikimuonyesha meneja huyo akimtuma kipa wake wa akiba Jerzy Dudek kupeleka ujumbe kwa kipa chaguo la kwanza Iker Casillas ambae nae aliufikisha ujumbe huo kwa Sergio Ramos na kisha baada ya muda vitendo vya kuonyesha kadi vilichukua mkondo wake.
UEFA wametoa siku tatu kwa watuhumiwa hao kukata rufaa endapo wataona wameonewa kwa maamuzi yaliyotolewa dhidi yao.
Hii si mara ya kwanza kwa, UEFA kutoa adhabu baada ya kubaini kuna udanganyifu wa kutafuta kadi za makusudi, kwani walishawahi kufanya hivyo msimu uliopita kwa wachezaji wawili wa klabu ya Olimpic Lyon ya nchini Ufaransa ambao ni Cris pamoja na Juninho walioonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Fiorentina.
Wachezaji wao walitozwa faini ya Euro 15,000 sambamba na kutokucheza mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Bayern Munich.
No comments:
Post a Comment