KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 2, 2010

JOE COLE KUREJEA UWANJANI LEO.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza Joe Cole hii leo anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha klabu ya Liverpool ambacho kitashuka dimbani kuwania point tatu muhimu za michuano ya ligi ya barani Ulaya mbele Steaua Bucharest ya nchini Romania.

Kiungo huyo anatarajia kurejea uwanjani hii leo baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma manne yaliyiopita ambayo yalishuhudia wakiwa anauguza jeraha la nyama za paja ambalo alilipata kwenye mchezo dhidi ya Bolton Wanderers waliokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri toka kwa Liverpool.

Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amesema anatarajia kumuanzisha kiungo huyo katika mchezo wa hii leo na ana imani kubwa atatoa mchago wake ambao utakisaidia kikosi cha klabu hiyo kuzipata point tatu muhimu ambazo zitawavusha na kuingia katika hatua inayoafuata ya michuano hiyo.

Amesema alikua na wakati mgumu wa kufikiria suala la majeruhi linalomkabili kwa sasa lakini kurejea kwa Joe Cole kumemfariji na anaendelea kutumai Liverpool itafikia malengo yake kama yalivyopangwa toka mwanzoni mwa juma hili.

Liverpool watashuka katika uwanja wa ugenini hii leo huku wakiwa na matumaini ya wachezaji wao mahiri kama: Reina, Kelly, Wilson, Kyrgiakos, Aurelio, Lucas, Poulsen, Shelvey, Cole, Jovanovic, Babel.

Baadhi ya michezo mingine wa ligi ya barani Ulaya inayochezwa hii leo ni pamoja na:

Borussia Dortmund v Karpaty Lviv

CSKA Moscow v Lausanne Sports

CSKA Sofia v Besiktas

FC Utrecht v Napoli

Paris SG v Sevilla

Rapid Vienna v FC Porto

BATE Borisov v Dynamo Kiev

FC Sheriff Tiraspol v AZ Alkmaar

Palermo v Sparta Prague

PAOK Salonika v Club Bruges

Villarreal v Dinamo Zagreb

Michuano hiyo ya ligi ya ulaya usiku wa kuamkia hii leo imeendelea tena kwa baadhi ya michezo kuchezwa ambapo;


AA Gent 1-0 Levski Sofia

Atletico Madrid 2-3 Aris Salonika

FC Metalist Kharkiv 2-1 Debrecen

Hajduk Split 1-3 AEK Athens

Lech Poznan 1-1 Juventus

Man City 3-0 Red Bull Salzburg

Odense BK 1-1 Getafe

Rosenborg 0-1 Bayer Leverkusen

Sampdoria 1-2 PSV Eindhoven

Sporting 1-0 Lille

Young Boys 4-2 VfB Stuttgart

Zenit St Petersburg 3-1 Anderlecht

No comments:

Post a Comment