KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 4, 2010

Joleon Patrick Lescott ATAFUTA MLANGO WA KUTOKEA.


Beki wa kimataifa toka nchini Uingereza Joleon Patrick Lescott amesema anatafuta namna yoyote ya kuondoka huko Eastland yalipo makao makuu ya klabu yake kwa sasa Man City ambayo ilimsajili mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Everton.

Joleon Patrick Lescott amesema anatafua namna ya kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kuchoshwa na mazingira mabovu ambayo yanamnyima nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha kwanza cha Roberto Mancini.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 28 amebainisha wazi kwamba toka msimu huu ulipoanza amekua na mazingira magumu ya kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza hatua ambayo amekiri haimfurahishi hata kidogo.

Amesema mara kadhaa amekua akimridhisha meneja wake Roberto Mancini kwa kucheza vyema wanapokua mazoezini lakini hushangazwa pindi kikosi kinapotajwa jina lake huwa halipo katika orodha ya wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza na mara nyingi hujikuta akitupwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba.

Katika hatua nyingine Joleon Patrick Lescott ametoa kauli za kumlaumu wazi wazi meneja wa sasa wa klabu ya Man City Roberto Mancini ambae amemuelezea kama mtu asietaka kumpa nafasi kwenye kikiosi chake hivyo anaona bora atafute mbinu mbadala za kuondoka.

Amesema wakati wa utawala wa meneja alietimuliwa kazi klabuni hapo Mark Hughes ambae ndie alimsajili akitokea Everton kwa ada ya uhamisho wa Paund million 24, alikua akichezeshwa kila juma na aliisaidia sana klabu hiyo lakini kuwasili kwa Mancini imekua shubiri kwake ya kushindwa kutimiziwa malengo ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Mazingira ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwa beki huyo yanakuja kufuatia kuwepo kwa Vincent Kompany na Kolo Toure huku mbadala wa mabeki hao ni kinda la kimataifa toka nchini ubelgiji Dedryck Boyata.

Toka oktoba 17 wakati wa mchezo wa man city dhidi ya Blackpool beki huyo hajajumuishwa kikosini mpaka hii leo.

No comments:

Post a Comment