KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 4, 2010

JINAMIZI LA KUKOSA UENYEJI 2018.


Kizaazaa cha kukosa nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 kwa nchi ya Uingereza, kimeendelea kuikumba nchi hiyo baada ya kaimu wenyekiti wa chama cha soka Roger Burden kutangaza kuondoa jina lake kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.

Roger Burden ametangaza kuondoa jina lake huku akitoa sababu zilizoeleza kwamba hawezi kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama cha soka nchini Uingereza baada ya nchi hiyo kukosa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Mbali na sababu hiyo Roger Burden akaendelea kufunguka kwa kueleza wazi kinaga ubaga cha kingine ambapo kimemfanya aondoe jina lake ambapo amesema endapo angekua na mawazo ya kuendelea kuiwania nafasi hiyo kuchaguliwa, angekua karibu mno na shiriksiho la soka duniani FIFA ambalo limeingia kwenye vita kubwa na nchi ya Uingereza.

Amesema hayupo tayari kufanya kazi na shirikisho hilo ambalo amedai hawezi kuliamini tena kwa yale yaliyotokea mjini Zurich nchizi Uswz Desemba 2 mwaka huu.

Maamuzi hayo ya Roger Burden mwenye umri wa miaka 64 yanaonekana kwenda kinyume na ushauri uliotolewa jana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ambapo aliwataka waingereza wote kuwa watulivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Mbali na waziri mkuu kuwataka waingereza kuwa katika hali ya utulivu nae meneja wa klabu ya Blackpoll Ian Holloway ameendelea kuwataka waingereza wenzake kuwa katika hali hiyo huku wakitambua heshima waliyopewa ya kuwa wenyeji wa michezo ya Olimpic ya mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment