KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 30, 2010

MAANDALIZI YA CHAN YAANZA.


Timu ya taifa ya Angola iliyosheheni wachezaji wanaosukuma soka la nyumbani, hii leo imefunga safari kuelekea nchi zilizo chini ya Falme za kiarabu, kwa ajili ya maandalizi ya fainali za mataifa bingwa barani Afrika (CHAN) za mwaka 2011, zitakazochezwa nchini Sudan kuanzia Februari 11.

Timu hiyo ikiwa huko itacheza michezo mitatu ya kujipima nguvu ambapo katika mchezo wa kwanza itacheza na timu ya taifa ya Qatar, kisha itarejea tena uwanjani kupambana na timu ya taifa ya Iran na katika mchezo wa mwisho itapimana ubavu na timu ya taifa ya Saudi Arabia.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Luanda kabla ya kuianza safari ya kwenda nchini Qatar kocha mkuu wa timu ya taifa ya Angola Zeca Amaral amesema michezo hiyo ya kimataifa ya kirafiki itawasaidia wachezaji wake kujenga mazingira mazuri ya kupambana vilivyo watakapokua kwenye michuano ya CHAN huko nchini Sudan mwaka 2011.

Amesema asilimia kubwa wachezaji wake hawana uzoefu wa kutosha wa kucheza na nchi za barani Asia hivyo, matarajio yake ni kuona suala hilo wanaliepuka na kujenga mikakati ya kupambana na timu kama Senegal, Rwanda pamoja na Tunisia waliopangwa nao pamoja katika kundi moja.

Kikosi cha Angola kilichosafiri hii leo kina wachezaji kama Lambito, Amaro, Fabrício, Pataca, Mingo Bille, Chará, Vado, Daniel Mpelepele, Santana Carlos pamoja na Rasca.

Wengine ni Wilson, Nuno, Kaly, Dani Massunguna, Miguel, Nary, Mabina, Hugo, Adawa, Job pamoja na Love Cabungula.

Makundi mengine ya michuano ya CHAN yamepangwa kama ifuatavyo.

Group A: Sudan, Gabon, Uganda, Algeria

Group B: Ghana, Afrika kusini, Zimbabwe, Niger

Group C: DR Congo, Cameroon, Cote d’Ivoire, Mali

No comments:

Post a Comment