KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 30, 2010

Carlo Ancelotti ATAMBA KUTETEA UBINGWA BAADA YA USHINDI.


Ushindi wa bao moja kwa sifuri uliopatikana jana kwenye uwanja wa Stamford Bridge umempa jeuri kubwa meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti ambae ametamba kikosi chake kimerejea katika mbio za ubingwa msimu huu.

Carlo Ancelotti ambae amekishuhudia kikosi chake kikipata ushindi wa kwanza mara baada ya kusota ndani ya michezo sita iliyopita amesema matokeo mazuri waliyoyapata jana ana imani yatakiongezea chachu kikosi chake ambacho mwishoni mwa juma hili kitakua nyumbani kikicheza na Aston Villa.

Amsema ushindi huo umewarejesha katika nafasi ya nne na kuwafanya kuwa nyuma kwa tofauti ya point nne dhidi ya vinara wa msimamo wa ligi Man Utd ambao wameshajikusanyia point 38 mpaka hivi sasa.

Carlo Ancelotti pia ametoa siri ya mafanikio ya ushindi huo ambapo ameeleza wazi kwamba kabla ya mchezo dhidi ya Bolton walikutana na bosi wao Roman Abramovich na kuzungumza masuala mbali mbalia mbayo anaimani yalikua sababu nyingine ya mafamnikio.

No comments:

Post a Comment