KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 30, 2010

Mick McCarthy AVUNJA MWIKO ULIODUMU KWA MIAKA 26.


Meneja wa klabu ya Wolves Mick McCarthy ameshindwa kuficha hisia zake za furaha alipohojiowa mara baada ya mchezo huo kumalizika ambapo alisikika akisema, mashabiki wengi walikidharau kikosi chake baada ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita mbele ya Wigan.

Amesema ushindi huo wa bao moja kwa sifuri walioupata jana licha ya kuwa ushindi wao wa kwanza toka mwezi March mwaka huu, bado unaendelea kuwapa chachu ya kujifikiria ni vipi wataweza kufanya vyema kwenye mchezo ujao dhidi ya Wet Ham Utd.

Mick McCarthy pia akazungumzia kufurahishwa na hatua ya kikosi chake kuvunja mwiko wa kufungwa na Liverpool ambayo imewanyanyasa kwa kipindi cha miaka 26 iliyopita.

No comments:

Post a Comment