KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 30, 2010

ACHENI KUWAZOMEA VIJANA WANAPOKUA SHUGHULINI.


Meneja wa klabu Liverpool Roy Hodgson ametoa wito kwa mashabiki wa klabu hiyo kuacha kasumba ya kukizomea kikosi chao kinapokua kikicheza katika uwanja wa nyumbani, hatua ambayo ameielezea huenda ikawa chanzo cha wao kuendelea kufanya vibaya.

Roy Hodgson ametoa wito huo baada ya kuonyesha kuchukizwa na vitendo vya kikosi chake kuzomewa na mashabiki ambao walidiriki kufanya hivyo kutokana na kuchukizwa na mwenendo wa kikosi hicho unavyokwenda.

Hodgson mwenye umri wa miaka 63 bado anaamini mashabiki wa Liverpool wanaendelea na wataendelea kukipenda kikosi chao licha ya kufanya vibaya katika mchezo wa jana dhidi ya Wolves ambao waliondoka mjini Liverpool na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Hata hivyo mzee huyo wa kiingereza amekiri kikosi chake jana kilicheza chini ya kiwango hali ambayo anaamini ilisababisha mwanya kwa wapinzani wao kutumia makosa hayo kujinyakulia point tatu muhimu.

No comments:

Post a Comment