KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 31, 2010

Ricardo Kaka KUREJEA TENA UWANJANI J3.


Mabingwa wa zamani wa barani Ulaya Real Madrid, mwanzoni mwa juma lijalo wanatarajia kurejea tena uwanjani kuendelea na ligi kuu ya soka nchini Hispania ambayo ilisimamam kupisha sikuku za mwishoni mwa mwaka.

Real Madrid wanarejea uwanjani huku wakichagizwa na taarifa njema za kurejea kwa kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil Rocardo Kaka ambae huenda akajumuishwa katika kikosi kitakachocheza na Getafe siku ya jumatatu.

Kaka alikua nje kwa miezi mitano iliyopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wake wa kushoto, na siku za hivi karibuni alianza mazoezi sambamba na wachezaji wenzake ambayo yamemshawishi meneja Jose Mourinho kumrejesha kikosini.

Mourinho amepata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari mjini Madrid Jose Mourinho amesema amefarijina na hatua ya kujea kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ambae amesema kwa hakika kurejea kwake kutakiongezea chachu kikosi chake ambacho kinasaka ubingwa wa nchini Hispania kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu kupita.

Mourinho pia ameonyesha masikitoko ya kuendelea kumkosa mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Argentina, Gonzalo Higuain ambae bado anakabiliwa na majeraha.
Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno pia ameweka wazi mipango yake ya kupanga utaratibu tofauti wa safu yake ya ulinzi ambayo itamkosa Pepe pamoja na Ricaldo Cavalho ambao wote kwa pamoja wanatumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Amesema anatarajia kuwatumia mabeki Raul Aibiol pamoja na Sargio Ramos katika nafasi ya ulinzi wa kati.

Levante pamoja na Real Madrid wanatarajia kukutana siku ya jumatatu huku wote kwa pamoja wakiwa na kumbu kumbu ya kupata ushidni katika michezo iliyopita, ambapo kwa upande wa The Merrenguess waliwachapa Sevilla bao moja kwa sifuri huku Getafe wakiwabanjua Almeria mabao matatu kwa mawili.

No comments:

Post a Comment