KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 15, 2011

ABRAMOVIC AMCHIMBA MKWARA MTALIANO.


Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amemueleza wazi meneja wa kikosi chake Carlo Ancelotti kufunga mkwiji kama anahitaji kuendelea kuwepo huko Stamford Bridge.

Ujumbe huo kwa Carlo Anceloti umekuja baada ya mmiliki huyo kuchoshwa na matokeo mabovu ambayo yamekua yakikiandama kikosi cha The Blues toka mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.

Abramovich, ambae kwa sasa yupo mapumzikoni huko n St Barts, nchini ufaransa inadaiwa alimpigia simu Anceloti na kumpa ujumbe huo, ambao pia yeye binafsi amekiri kuupokea kwa mikoni miwili na kuahidi kuufanyia kazi.

No comments:

Post a Comment