KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 15, 2011

Avran Grant KUFUNGASHIWA KILICHO CHAKE.


Wakati mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kati ya West Ham utd dhidi ya Arsenal ukitarajiwa kuchezwa muda si mrefu kuanzia sasa kwenye uwanja wa upton Park, imeelezwa kuwa huenda meneja wa wagonga nyundo hao Avram Grant akafungashiwa virago mara baada ya mtanange huo kumalizika.

Taarifa hizo zipo kama hazipo, zimejitokeza kwenye magazeti mengi hii leo nchini Uingereza ambapo imeelezwa kwamba nafasi ya meneja huyo wa kimataifa toka nchini Israel huenda ikachukuliwa na aliekua meneja wa klabu ya Aston Villa msimu uliopita Martin O'Neill.

Sababu kubwa ya Avran Grant kufikiriwa kuondoka klabuni hapo ni kufuatia matokeo mabovu yanayomuanda toka mwanzoni mwa msimu huu ambapo mpaka sasa kikosi chake kina point 20 baada ya kushika dimbani mara 22.

Hata hivyo licha ya kuwepo kwa taarifa hizo za uwezekano wa Grant, kutimuliwa kazi klabuni hapo, wachezaji wake, wameahidi kufanya kila juhudi za kumlindia kibarua chake wakianzia kwenye mchezo wa hii leo baada ya kufanya kwenye kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi, pale walipoichapa Birmingham city mabao mawili kwa moja siku ya jumanne ya juma hili.

Avram Grant alikabidhiwa kikosi cha West ham utd mwanzoni mwa msimu huu akichukua nafasi ya Gianfranco Zola toka nchini Italia aliefanikisha utaratibu wa kukinusuru kikosi hicho cha Upton Park kutokushuka daraja msimu uliopiata.

No comments:

Post a Comment