KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 10, 2011

ARSENAL KUSAJILI BEKI MWEZI HUU.


Mkuu wa jeshi la Ashburton Grove Arsène Charles Ernest Wenger, huenda akaingia sokoni kufanya usajili wa mchezaji mmoja kufuatia taarifa za kuumia kwa beki wake wa kimataifa toka nchini Ufaransa Sebastien Squillaci.

Wenger anategemea kufanya usajili wa mchezaji huyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye jopo la madaktari huko Emirates ambazo zimeeleza Sebastien Squillaci amapata maumivu makali ya nyonga hivyo huenda ikamchukua muda mrefu kurejea katika hali yake ya kawaida.

Mzee huyo wa kifaransa amesema kutokana na taarifa hizo, kikosi chake kwa sasa kinasaliwa na mabeki wawili wa kati hivyo hana budi kufanya usajili wa beki mwingine ili kuziba nafasi iliopo.

Tayari taarifa zimeshaanza kuzagaa ambapo inadaiwa kwamba Arsene Wenger anatazamiwa kumsajili beki wa kati wa klabu ya Bolton Wanderers Garry Cahill ambae amekuwa akifuatiliwa na mzee huyo mwenye umri wa miaka 61 kwa muda mrefu uliopita.

Kuumia kwa Sebastien Squillaci, kunamfanya ajiunge na beki mwingine alie majeruhi Thomas Vermaelen ambae mwishoni mwa mwezi huu Anategemea kurejea kundini kujiunga na mabeki wenzake Laurent Koscielny pamoja na Johan Djourou.

Katika kipindi hiki Arsenal wanakabiliwa na mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Carling dhidi ya Ipswich Town, mchezo wa marejeano wa kombe la FA dhidi ya Leeds Utd, michezo ya ligi pamoja na mchezo wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona hivyo wanahitaji kuziba nafasi hiyo ya ulinzi haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment