Chama cha soka nchini Ghana GFA kimetimiza ndoto ya kikosi cha timu ya taifa hilo kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
GFA wametimiza ndoto hiyo baada ya kuwasilisha maombi ya mchezo huo siku kadhaa zilizopita na hii leo chama cha soka nchini Uingereza kimethibitisha kuyakubali maombi hayo na kutaja tarehe ya pambano hilo.
Taarifa iliyotolewa na FA ya nchini Uingereza imeeleza kwamba mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki utachezwa March 29 mwaka huu.
Nchi hizo ambazo zote kwa pamoja zilishiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2010 huko nchini Afrika kusini zitavikutanisha vikosi cha wachezaji wakubwa kwa mara ya kwanza katika historia ya mchezo wa soka, huku kumbu kumbu ikionyesha kwamba nchi hizo zimekua zikikutana kwenye michuano ya vijana.
Katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2009 timu ya taifa ya vijana ya Ghana ilifanikiwa kuifumua timu ya taifa ya Uingereza mabao manne kwa sifuri, na katika fainali za vijana chini ya umri wa miaka 18 timu ya taifa ya Uingereza ilifanikiwa kuifunga Ghana mwaka 2007.
Katika mchezo huo kiksoi cha Ghana kinatarajiwa kuwa na wachezaji mashuhuri kama Michael Essien, John Pantsil, Asamoah Gyan, Richard Kingston pamoja na John Mensah ambao wanacheza katika ligi ya nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment