KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 15, 2011

ARSENAL MWENDO MDUNDO.

West Ham United 0-3 Arsenal


Ligi hiyo yataraji kuendelea tena kesho, ambapo mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa ni ule utakaowakutanisha mahasimu wawili wa jiji la Liverpool, Everton dhidi ya wajogoo wa jiji.

Meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish amesema wanakwenda katika mchezo huo wa kesho huku wakitambua tayari wameshafanya makosa ya kukubali kupoteza michezo mingi lakini bado wana nafasi ya kurekebiosha makosa hayo.

Dalglish pia amezungumzia msimu wa dirisha dogo la usajili uamnondelea hivi sasa huko barani Ulaya kwa kusema hafikirii kumuuza mchezaji hata mmoja licha ya vyombo vya habari kueleza kuwa baadhi yaw a wachezaji wa klabu hiyo ya Anfield.

Nae meneja wa klabu ya Everton David Moyes amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo wa kesho huku akikumbushia kasi yao ya ajabu waliyoionyesha katika mchezo uliopita wa ligi kwa kuitandika tottenham hotspurs.

Moyes pia akazungumzia masikitiko yake kufuatia kuondoka kwa Roy Hodgson na kukaribishwa na Kenny Dalglish ambae amedai anamuheshimu toka walipokua akisakata kabumbu.

MICHEZO MINGINE ITAKAYOCHEZWA KESHO NI PAMOJA NA.

Birmingham v Aston Villa

Sunderland v Newcastle

Tottenham v Man Utd

No comments:

Post a Comment