KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 12, 2011

Avram Grant AONYESHA TABASAMU BAADA YA USHINDI.



Katika hali ya kustaajabisha, meneja wa klabu ya West Ham Utd Avram Grant usiku wa kuamkia hii leo alionyesha sura ya kutabasamu baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Birmingham City.

Grant alionyesha hali hiyo alipozungumza na vyombo vya habari ambapo aliwashangaza waandishi wengi waliokua wamehuhdhuria kwenye ukumbi wa mikutano huko Upton Park.

Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Israel amesema ushindi wa mabao mawili kwa moja uliopatikana katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi dhidi ya Birmingham City umekiweka kikosi chake katika mazingira mazuri ya kutinga katika hatua ya fainali.

Nae meneja wa klabu ya Birmingham City Alex McLeish amezungumzia masikitiko ya kupoteza mchezo huo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ambao tayari ulikua umeshaonyesha ishara ya matokeo ya sare kabla ya Bemn Foster kufanya makosa kipindi cha pili.

Amesema kilichosalia hivi sasa ni kujipanga kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali utakaochezwa mjini Birmingham kwenye uwanja wa St Andrew.

Hii leo michuano hiyo ya kombe la ligi inaendelea kwa mchezo mwingine wa hatua ya nusu fainali, kupigwa huko Potman road ambapo jeshi la Ashburton Grove Arsenal litakaribishwa na wenyeji wao Ipswich Town.

No comments:

Post a Comment