KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 12, 2011

Steven Garrard AKUMBUKWA LIVERPOOL.


Meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish ameeleza wazi hisia zake za machungu ya kumkosa nahodha na kiungo wa klabu hiyo Steven Garrard kwenye michezo mitatu ijayo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Dalglish ameelezea hisia hizo zikiwa zimebaki saa kadhaa kabla ya kikosi chake kurejea tena uwanjani kucheza mchezo wa kiporo cha ligi kuu dhidi ya Blackpool huko Bloomfield Road.

Amesema kwa kipindi hiki kigumu kwa kikosi chake bado kuna umuhimu wa kuwepo kwa mchezaji huyo lakini kutokana na mazingira yaliopo hana budi kukubali kuendelea kumkosa.

Amesema mchezo wa hii leo ni muhimu sana kwao hivyo inamlazimu kufanya jitihada binafsi ambazo zitamuwezesha kuziba pengo la Steven Gerrard ambae alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Man Utd mwishoni mwa juma lililopita.

Mchezo wa Liverpool dhidi ya Blackpool analazimika kuchezwa hii leo baada ya kuahirishwa mwishoni mwa mwaka uliopita kufuatia hali ya hewa ambayo ilisababisha michezo mingine kusogezwa mbele.

No comments:

Post a Comment