KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 7, 2011

BADO TUPO KWENYE MBIO ZA UBINGWA.


Meneja msaidizi wa klabu ya Man City Brian Kidd amesema bado kikosi cha klabu hiyo kipo kwenye harakati za kusaka ubingwa wa soka nchini humo, licha ya kuonyesha mchezo mbovu mbele ya Arsenal siku mbili zilizopita.

Brian Kidd amesema haoni sababu ya kikosi cha klabu hiyo kuondoshwa katika mbio za ubingwa msimu huu kwa kisingizio cha kucheza mchezo wa kujihami huko Emirates, ambapo walionekana kuzidiwa kwa kiasi kikubwa na wenyeji wao.

Amesema kwa sasa kikosi chao kinaonyesha ukomavu wa hali ya juu na hatua hiyo ndio inawapa jeuri ya kusema bado wapo kwenye mbio za ubingwa, huku wakiwa nyuma ya Man utd walio kileleni kwa tofauti ya point mbili.

No comments:

Post a Comment