KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 7, 2011

KITI MOTO CHA Roy Hodgson KILA MMOJA ASEMA YA KWAKE.


Licha ya taarifa kuendelea kueleza kwamba huenda Roy Hodgson akatimuliwa kazi wakati wowote na uongozi wa ngazi za juu wa klabu ya Liverpool, wito umetolewa kwa mashabiki wa klabu hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha endapo wanahitaji matokeo mazuri.

Wito huo kwa mashabiki wa klabu ya Liverpool ambao kwa michezo kadhaa wameonyesha kuchukizwa na mwenendo wa kikosi chao umetolewa na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo John Barnes, Kelvin Kigaan pamoja na Steve Mcmanaman.

Wachezaji hao wa zamani kwa nyakati tofauti wamelizungumzia suala hilo ambapo kwa upande wa John Barnes aoliekuwepo huko Anfield kuanzia mwaka 1987-97 amesema hakuna siri ya kupatikana kwa ushindi klabuni hapo zaidi ya kutoa ushirikiano kwa meneja Roy Hodgson ambae anaamini bado ana uwezo wa kutosha wa kuikoa Liverpool.

Kevin Keegan aliekitumikia kikosi cha The Reds kuanzia mwaka 1971-77 yeye amegusia suala hilo kwa upande wa uongozi ambapo ameutaka kuhakikisha unatoa nafasi ya upendeleo kwa mzee huyo, kufuatia mahitaji anayoyahitaji katika kipindi hiki cha usajili kwa lengo la kupata wachezaji watakaokiboresha kikosi chake.

Steve Mcmanaman aliekitumikia kikosi cha Liverpool toka mwaka 1990-99 ameomba Hodgson kupewa muda wa kujipanga zaidi hasa ukizingatia amekichukua kikosi mwanzoni mwa msimu huu kikiwa kina mapungufu makubwa kwa baadhi ya wachezaji kuondoka na wengine kuwa majeruhi kwa sasa hivyo amesisitiza suala hilo la muda ambalo anaimani ni suluhisho tosha.

Roy Hodgson yupo kwenye wakati mgumu kufuatia mambo kuzidi kumuendea kombo katika harakati za kurejesha heshima ya klabu ya Liverpool iliyopania kumaliza kwenye nafasi nne za juu ili iweze kucheza michuano ya ligi ya mbaingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment